Siddhārtha Gautama (kwa Kisanskrit: सिद्धार्थ गौतम; kwa Kipali: Siddhattha Gotama) alikuwa mwalimu wa kiroho kutoka India.
Kutokana na mafundisho yake, ulianzishwa Ubuddha ambao unatazamwa kwa kawaida kuwa dini.[1] Katika mapokeo mengi ya Kibuddha anatazamwa kama Buddha mkuu (P. sammāsambuddha, S.samyaksaṃbuddha) wa wakati wetu, ambapo "Buddha" maana yake ni "aliyeamshwa" au "aliyeangazwa." [2]
Miaka yake ya kuishi haina hakika: wanahistoria wengi wa mwanzo wakarne ya 20 walitaja miaka 563 KK hadi 483 KK hivi,[3] lakini maoni ya siku hizi yanataja mwaka wa kufariki kati ya 486 KK na 483 KK au, hata kati ya411 KK na 400 KK.[4][5]
Kadiri ya akiolojia, Buddha aliweza kuzaliwa huko Lumbini, (leo nchiniNepal)[6][7][6] au huko Kapilavastu, Piprahwa, Uttar Pradesh, India au tena Kapileswara, Orissa, India.[8][9][10][11][12]
Gautama, anayejulikana pia kama Śākyamuni ("Mwenye hekima wa Śākyas").
JOIN OUR FACEBOOK GROUP :https://m.facebook.com/groups/1425281167771729
Contribute Translations ;
No comments:
Post a Comment